Breaking News

Nicki Minaj kuwalipia karo mashabiki wake Marekani


Mwanamuziki Nicki Minaj ameahidi kulipia karo baadhi ya mashabiki wake.
Hata hivyo amesema ni lazima wathibitishe kwamba walipata alama A katika mtihani wao wa kujiunga na vyuo.
Alikuwa akijibu maombi kutoka kwa mashabiki wake kwenye Twitter ambao walitaka awape pesa.
Baada yake kusema atasaidia wale waliopata alama A, baadhi walimtumia kwenye Twitter picha za matokeo yao ya mtihani na kumweleza matatizo ya kifedha yanayowakabili.

Wengi walikuwa wanaomba msaada wa chini ya $1,000 (£770) lakini katika kisa kimoja, alionekana kuwa tayari kutoa msaada wa $6,000 (£4600) kwa mwanafunzi mmoja, iwapo angethibitisha anataka kuzitumia wka njia gani.

Shabiki huyo kwa jina Josh alisema pesa hizo ni za karo, malazi, chakula na vitabu.
Alitania kwamba asipokosa kutoa msaada, basi atabaki mwenyewe bila pesa.
Kwa jumla, amejitolea kuwasaidia mashabiki 30.
Mapema mwana huu, mwanamuziki huyo alitoa $1m (£870,00) zakusaidia shule mjini Chicago.
"Hatua hii si ya kujifaidi kisiasa, si ya kujionyesha, ni ya kuwajali na kuwatunza watoto," alisema wakati huo, na kutoa wito kwa mashirika mengine na kampuni Chicago kusaidia wasiojiweza.


No comments